Watu 22 waokolewa baada ya jengo la kanisa kuporomoka nchini Uganda

(CRI Online) Oktoba 27, 2026

Polisi wa Uganda wamesema takriban watu 22 wameokolewa baada ya jengo la kanisa lililokuwa likijengwa kuporomoka jana jioni huko Wakiso, katikati mwa Uganda.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, jengo lililoporomoka lilikuwa ni sehemu ya upanuzi ya jengo kuu la kanisa huko Bwerenga mjini Katabi.

Polisi wamesema shughuli za uokoaji zinaendelea, na hadi sasa takriban watu 22 wameokolewa na kuhamishwa kwenye hospitali ya Daraja la B ya Entebbe kwa matibabu.

Timu za dharura zilikuwa zikiendelea na juhudi za utafutaji na uokoaji, na serikali ya huko inafanya kazi kuhakikisha kama kuna watu zaidi wamenaswa chini ya kifusi au la.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha