Lugha Nyingine
Maonesho ya mitindo yaliyofadhiliwa na China yahimiza utalii na utamaduni wa Ethiopia

(Picha/Xinhua)
Maonesho ya mitindo yaitwayo “Uso wa Ethiopia” yaliyofadhiliwa na kampuni moja ya China, yalifanyika kwa mafanikio Jumapili Oktoba 25 mjini Addis Ababa, ambapo washiriki walionesha na kutangaza utamaduni, urithi, mila na vivutio vya kitalii vya Ethiopia.
Washiriki 20 walifika hatua ya fainali iliyoandaliwa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya Ethiopia kwa kushirikiana na kampuni ya masuluhisho ya nishati safi na endelevu ya G-Power Manufacturing PLC, iliyowekezwa na China.
Ma Ning, ofisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, amesema kampuni yake ina ruwaza ya kukuza sekta ya utalii nchini Ethiopia na kutoa fursa nyingi zaidi kwa mawasiliano ya kitamaduni na kitalii kati ya China na Ethiopia.
Akiongea kwenye tukio hilo, waziri wa nchi anayeshughulikia utamaduni na utalii, Endegena Abebe, ameishukuru kampuni hiyo kwa kuhimiza utamaduni na utalii wa Ethiopia kupitia mbinu na burudani za kidijitali, akisisitiza haja ya Ethiopia kuiga mfano huo na kuendeleza juhudi kwenye ujenzi wa taswira na kutangaza utamaduni wake mkubwa kupitia teknolojia za kisasa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



