Kamati Kuu ya 20 ya CPC yaanza mkutano wa tano wa wajumbe wote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 27, 2026

BEIJING - Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imeanza mkutano wake wa tano wa wajumbe wote mjini Beijing jana Jumatatu asubuhi, ambapo Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping alitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, na kufafanua mswada wa azimio la Kamati Kuu ya CPC juu ya masuala muhimu yanayohusu kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote.

Mswada huo wa azimio unafanya majumuisho ya mafanikio na uzoefu wa kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote katika zama mpya kwa kufuata msimamo wa kutafuta ukweli kutokana na hali halisi, na pia umetoa uchambuzi wa kina kuhusu hali na majukumu ya ujenzi wa Chama kwa hivi sasa na katika kipindi kijacho.

Kutokana na taarifa ya mkutano wa Ofisi ya Siasa uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu, ambao uliamua waraka wa mswada huo wa azimio utawasilishwa na kuthibitishwa kwenye mkutano wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama, mswada huo wa azimio pia umetoa mipango ya mikakati ya kuimarisha kazi ya kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote, na kusisitiza kushikilia kufanya kazi hii bila kulegalega.

Mkutano wa Ofisi ya Siasa uliofanyika mwezi Julai mwaka huu, ambao uliamua ajenda za mkutano wa tano wa wajumbe wote wa kamati kuu ya Chama, ulieleza kuwa, tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwaka 2012, maendeleo makubwa yamepatikana katika kazi ya kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote, hali ambayo imeanzisha hali mpya kwa Chama hicho chenye umri wa miaka 100 katika kujifanyia mageuzi, na kuleta mafanikio ya kihistoria na mabadiliko makubwa katika mambo ya Chama na maendeleo ya nchi.

Mkutano huo ulisema kuwa Chama na wananchi wameshinda katika mpango wa kihistoria wa kujenga Chama na nchi vyenye nguvu, lakini ulidhihirisha kuwa kutokana na mabadiliko makubwa yanayotokea duniani, nchini China na ndani ya Chama, juhudi za kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote pia zinakabiliwa na hali mpya nyingi na changamoto.

Mkutao huo umetoa wito wa kufuata vigezo vya juu zaidi na kuchukua hatua halisi zaidi kwa kudumisha na kutumia uzoefu wa thamani wa kujiendesha Chama kwa nidhamu kali kwa pande zote katika zama mpya, kutatua matatizo makubwa katika ujenzi wa Chama, na kuimarisha na kuendeleza mazingira mazuri ya kisiasa yaliyojengwa kupitia Chama kujisimamia na kujiendesha chenyewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha