Wasanii Wachora Mustakabali wa Pamoja wa Asia na Pasifiki katika Kijiji cha Kale cha Wahakka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2026

Kituo cha Sanaa ya Uchapaji cha Guanlan mjini Shenzhen, China, kimefanya ukarabati na kuhifadhi nyumba zaidi ya 20 za jadi za Wahakka zilizojengwa karibu miaka 300 iliyopita. Kazi hii imewezesha utamaduni wa Wahakka na sanaa ya uchapaji kutoka nchi mbalimbali kukutana na kufungamana.

Tangu kilipoanzishwa, kituo hicho kimepokea wasanii zaidi ya 2,000 kutoka nchi na maeneo zaidi ya 100 kuishi na kufanya kazi za sanaa.

Kwa sasa, shughuli za sanaa ya uchapaji zenye kaulimbiu ya “Sanaa ya Uchapaji ya Pamoja kwa Mustakabali wa Asia na Pasifiki” zinafanyika katika kijiji hicho. Shughuli hizo zimewaalika wasanii kutoka nchi na maeneo wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) kubuni na kuunda kazi za uchapaji zinazohusu maendeleo ya kijani, uvumbuzi wa kidijitali, na mawasiliano ya utamaduni.

Kupitia utaratibu wa kudumu wa kubadilishana uzoefu na wasanii wa kimataifa, kituo cha Guanlan kinahifadhi mandhari ya mashambani ya Lingnan na kuendeleza utamaduni wa Wahakka. Wakati huohuo, kinatoa jukwaa la kimataifa la kubadilishana uzoefu wa sanaa lenye sifa za Mashariki.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha