Libya yamwita kaimu balozi wa Marekani, yamlaani kwa kutoa "maneno ya kuudhi"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 26, 2026

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya Jumapili ilisema kuwa, imemwita kaimu balozi wa Marekani nchini Libya, na kupinga rasmi "maneno ya kuudhi" dhidi ya Libya na wananchi wake.

Wizara hiyo ilisema imewasilisha taarifa rasmi ya upingaji kwa mwanadiplomasia huyo, ikitaka ufafanuzi na marekebisho rasmi vitolewe juu ya maneno husika yaliyosemwa.

Wizara hiyo ilisisitiza kuwa inapinga maneno yoyote yanayodhuru heshima ya wananchi wa Libya, na pia inapinga kuifanya Libya kuwa shabaha la mizozo ya uchaguzi na lengo la hila za kisiasa nchini humo.

Rais wa Marekani Donald Trump, alipotoa hotuba kwenye mkutano wa hadharani wa kampeni ya uchaguzi katika Jimbo la Georgia Jumamosi, alikosoa vikali sera kuhusu wahamiaji, na kusema kuwa Libya, Yemen, Haiti na Somalia ni "nchi zenye hali ya ugaidi unaokithiri".

Maneno hayo yamesababisha lawama nyingi za wanasiasa na katika maoni ya umma nchini Libya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha