Lugha Nyingine
China yafanya shughuli za kumbukumbu za Miaka 81 ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan

Picha hii ikionyesha stempu ya ukumbusho iliyochapishwa na Kampuni ya Posta ya China kwa kumbukumbu za Siku ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan. Kampuni ya Posta ya China jana Jumapili ilitoa stempu hiyo yenye picha ya Ukuta Mkuu, Mlima wa Alishan na Ziwa la Jua na Mwezi, na imewavutia sana wakusanyaji stempu katika vituo vya posta vya China Bara na majukwaa ya mtandaoni. (Xinhua)
Jana Jumapili, China iliadhimisha miaka 81 ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan na siku ya ukumbusho wake, ambapo shughuli zilifanyika kwenye pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, ili kukumbuka historia ya mapambano ya pamoja dhidi ya uvamizi wa Japani, na kusisitiza wito wa muungano wa taifa.
Kongamano lilifanywa mjini Fuzhou, Mkoa wa Fujian, China, watu 200 hivi walishiriki kwenye kongamano hilo, wakiwemo pamoja na watu wa vizazi vya wapiganaji wa Taiwan waliopinga uvamizi wa Japan na mashujaa wa mapinduzi, vijana kutoka pande zote mbili za Mlango-Bahari wa Taiwan, wajumbe kutoka Hong Kong, Macao, na wakazi wa ng'ambo, pamoja na wataalamu na wasomi.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Kazi ya Taiwan ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na pia Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China Bw. Song Tao alisema katika kongamano hilo kwamba, kuwekwa kwa Siku ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan kumeonesha nia thabiti ya China ya kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake, na pia kunasaidia kuimarisha maoni ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa kuhusu kulinda kanuni ya kuwepo kwa China moja.
Baada ya vita dhidi ya China mwaka 1894, Japan ilikalia Taiwan na Visiwa vya Penghu mwaka 1895, na kuifanya Taiwan iwe chini ya utawala wa kikoloni kwa miaka hamsini. Kujitoa kwa Taiwan kutoka utawala wa kikoloni wa Japan mwaka 1945 kulionesha ushindi wa wananchi wa China wa mapambano magumu ya kijasiri dhidi ya uvamizi wa Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, na pia ni wakati muhimu kwa China kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi yake.
Mnamo Oktoba 2025, Bunge la Umma la China (NPC) liliweka tarehe 25 Oktoba kuwa Siku ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan.
Siku ya Jumamosi iliyopita, Kamati Kuu ya Shirikisho la Kujitawala la Kidemokrasia la Taiwan lilifanya shughuli za kumbukumbu kwenye uwanja wa ukumbusho ulioko kitongoji cha magharibi cha Beijing. Washiriki walisimama kimya kwa heshima, wakaimba na kuweka maua kuwakumbuka mashujaa waliojitolea mihanga kwa ajili ya muungano wa taifa.
Xu Yunchu, mjukuu wa shujaa wa mapinduzi Zhu Feng, alisema historia ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan inathibitisha kwamba Taiwan ni sehemu ya China isiyoweza kutenganishwa.

Picha hii ikionyesha stempu ya ukumbusho iliyotolewa na Kampuni ya Posta ya China kuadhimisha Siku ya Taiwan kujitoa kutoka utawala wa kikoloni wa Japan. (Xinhua)

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma