Lugha Nyingine
Shughuli ya Jukwaa la Mtaa wa Fedha yafanyika sambamba nchini Kenya kwa mara ya kwanza, kulenga kuhimiza ushirikiano

Tarehe 21 Oktoba 2026, John Mbadi, Waziri wa Fedha na Mpango wa Uchumi wa Kenya, akihutubia Jukwaa la Satelaiti la Nairobi la Mkutano wa Mwaka wa 2026 wa Jukwaa la Mtaa wa Fedha huko Nairobi, Kenya, (Xinhua/Ni Yuanshi)
Siku ya Jumatano Kenya iliandaa jukwaa la ngazi ya juu lililowaalika maofisa waandamizi wa serikali, taasisi za mambo ya fedha na washirika wa maendeleo kutoka nchi za Afrika na China, likilenga kufungua fursa mpya za uwekezaji na ufadhili chini ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".
Shughuli hii ni Jukwaa la Satelaiti la Nairobi la Mkutano wa Mwaka wa 2026 wa Jukwaa la Mtaa wa Fedha. Hii ni mara ya kwanza kwa jukwaa hilo la Mtaa wa Fedha kuandaa shughuli barani Afrika.
Shughuli hiyo liliandaliwa kwa pamoja na Benki ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa za China na Wizara ya Fedha ya Kenya, ikiwa na kaulimbiu "Kushikilia Ufunguaji Mlango na Ushirikiano na Kutia Nguvu Mpya Ushirikiano wa Sifa Bora Katika Ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'", na ulifanyika sambamba na shughuli za Beijing kwa njia ya video.
John Mbadi, Waziri wa Fedha na Mpango wa Uchumi wa Kenya amesema, jukwaa hilo linaonesha urafiki wa kudumu na uhusiano imara wa washirika wa maendeleo kati ya Afrika na China, na limetoa jukwaa lenye thamani kubwa la kubadilishana mawazo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa uwekezaji na ufadhili ili kusukuma mbele maendeleo endelevu.
Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan amesema China na Afrika zinaingia katika kipindi kipya cha kuhimiza kwa pamoja maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa na ufunguaji mlango na ushirikiano unafanya kazi muhimu katika kukabiliana na changamoto za dunia nzima na kuhimiza maendeleo ya pamoja.
Wakati wa shughuli hii, mashirika ya China na Afrika yalitilia saini kwenye nyaraka nyingi za makubaliano (MoU) zilizolenga kupanua ushirikiano katika uwekezaji, urahisishaji wa biashara na ujenzi wa miundombinu chini ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

Tarehe 21 Oktoba 2026, wahudhuriaji wa mkutano wakishiriki kwenye Jukwaa la Satelaiti la Nairobi la Mkutano wa Mwaka wa 2026 wa Jukwaa la Mtaa wa Fedha huko Nairobi, Kenya. (Xinhua/Ni Yuanshi)

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma