Lugha Nyingine
Rais wa China atoa agizo la juhudi kubwa za uokoaji kufuatia tetemeko kubwa la ardhi kutokea mkoani Xizang
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 kwenye kipimo cha Richter limetokea jana katika Wilaya ya Baqen, mjini Nagqu mkoani Xizang, na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi.
Baada ya tetemeko hilo kutokea, rais Xi Jinping wa China ameagiza kufanya juhudi kubwa katika kazi ya utafutaji na uokoaji, na matibabu ya watu waliojeruhiwa, ili kupunguza idadi ya vifo na majeruhi kadiri iwezekanavyo.
Rais Xi amesisitiza kuwa eneo la maafa liko katika sehemu ya mwinuko wa juu lenye baridi kali, na inatakiwa kufuatilia kwa makini hali ya tetemeko na mabadiliko ya hali ya hewa, na kutekeleza kazi ya uokoaji kwa njia ya kisayansi, ili kuepuka maafa yanayoambatana na tetemeko. Pia inatakiwa kuharakisha kuandaa vifaa na riziki za uokoaji, kuwahamisha wakazi walioathiriwa, kukarabati miundombinu iliyoharibiwa, na kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma