Kutoka jangwa la manjano hadi “bahari ya bluu”: Teknolojia yajenga upya siku za baadaye za kijani za Kubuqi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2026

Katika Dalad Banner, Mji wa Ordos wa Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, safu za paneli za nishati ya jua zenye rangi ya bluu ambazo mwisho wake hauonekani zinazunguka kwa kufuata mwendo wa jua, kama kundi la farasi ambao wapo tayari kuanza mbio. Chini ya paneli hizo, mimea inayostahimili mazingira ya jangwani inastawi na kuzuia upepo na mchanga.

Jangwa hilo ambalo lilikuwa hakuna kitu chochote licha ya upepo mkali na mchanga wa manjano, hivi leo limepata njia ya maendeleo ya nishati mbadala, kurejesha hali ya ikolojia na kuwawezesha watu kuongeza vipato.

Mabadiliko haya kutoka jangwa la manjano hadi “bahari ya bluu” hayawezekani kutokea kwa nguvu ya upande mmoja peke yake, bali yametokana na juhudi za pamoja za mwongozo wa sera, uvumbuzi wa kiteknolojia na uzoefu na ushirikiano wa watu wa mashinani.

Hapo awali, watu walijenga kituo hicho kwa lengo la kuzalisha umeme kwa nishati ya jua tu, lakini kadiri uzoefu wao ulivyozidi kwa kina, waligundua hatua kwa hatua kumbe paneli za nishati ya jua zinaweza pia kuboresha hali ya hewa ya eneo dogo jangwani, na kuchochea urejeshaji wa ukuaji wa mimea.

Sui Limin, mkuu wa kituo cha uzalishaji wa umeme kwa nishati ya jua cha Dalad Banner, katika doria zake za ukaguzi za kila siku, ameshuhudia kutatuliwa kwa mfululizo wa matatizo magumu, ikiwemo kuchomeka nguzo katika mchanga unaohamahama, kuzuia upepo na kufunga mchanga, na uendeshaji wa kisasa; Nao wakulima na wafugaji wanaoshiriki katika mambo ya kilimo chini ya paneli, wamepita pia miaka yao ya “kuishi pamoja na upepo na mchanga”, wakishikilia imara “bakuli la riziki la ikolojia” lenye maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu Xi Jinping alisisitiza: “Tushikilie njia ya maendeleo ya ustaarabu ya kuendeleza uzalishaji, kuishi maisha bora na kuwa na mazingira mazuri ya ikolojia.” Kutoka kuzalisha umeme peke yake hadi maendeleo jumuishi ya “nishati ya jua + kudhibiti jangwa + viwanda”, uzoefu wa Kubuqi unathibitisha kwamba kupunguza umaskini si kushinda mazingira ya asili, bali ni kufikia kuishi pamoja na kupata ustawi kati ya binadamu na mazingira ya asili, na kati ya binadamu na viwanda kupitia sayansi na teknolojia.

Kwa kuelekea siku za baadaye , uzoefu wa China katika kudhibiti jangwa unaenezwa duniani kwa kasi, na China pia itashirikiana na nchi nyingine duniani kuunda miujiza zaidi ya maendeleo ya “kubadilisha jangwa kuwa oasisi”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha