Lugha Nyingine
Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Djibouti wakutana
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na mwenzake wa Djibouti Abdelkader Hussein Omar ambaye yupo ziarani nchini China.
Katika mazungumzo yao, Wang amesema chini ya uongozi wa kimkakati wa marais wa nchi hizo mbili, uhusiano wa China na Djibouti umedumisha mwelekeo wa maendeleo mazuri yenye utulivu. Ameongeza kuwa Rais wa China Xi Jinping ametoa kanuni nne kuhusu pande husika kushiriki kwenye utatuzi wa changamoto za Afrika kwa njia ya kiujenzi, na mapendekezo kadhaa ya kuhimiza amani na utulivu kwenye Mashariki ya Kati. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali ikiwemo Djibouti kulinda kihalisi amani na utulivu wa kikanda.
Naye Omar amesema Djibouti siku zote inafuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kupongeza mapendekezo yaliyotolewa na Rais Xi, na mchango uliotolewa na China katika kuhimiza amani ya kudumu duniani.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma