Rais Xi Jinping ahudhuria na kuhutubia Mkutano wa kuadhimisha Miaka 90 ya Ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu la China

(CRI Online) Oktoba 22, 2026

Mkutano wa Kuadhimisha Miaka 90 ya Ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu la China umefanyika asubuhi ya leo Oktoba 22 hapa Beijing. Rais Xi Jinping amehudhuria na kuhutubia mkutano huo.

Wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi, makamu wa rais Han Zheng pia wamehudhuria mkutano huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha