Lugha Nyingine
Kwaheri kamba ya kuteleza! Dada wawili wa Nujiang wavuka kuelekea maisha mapya
Bonde kubwa la Mto Nujiang katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Walisu la Nujiang, Mkoa wa Yunnan, kusini-magharibi mwa China, linajulikana kwa milima yake mirefu na mto unaotiririka kwa kasi.
Kwa vizazi vingi, kamba za kuteleza zilikuwa njia muhimu ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo.
Mwaka 2007, picha ya dada Yu Chunhua na Yu Caimei wakivuka mto kwa kamba ya kuteleza kwenda shule iliwagusa watu wengi sana.
Baada ya uzinduzi wa mpango wa China wa kubadilisha kamba kuwa madaraja, madaraja yalianza kuvuka Mto Nujiang, na kugeuza bonde la asili kuwa njia kuu ya kupita.
Hivi leo, tarafa ya Maji katika Wilaya ya Fugong imejenga madaraja 16 ya kuvuka mto, na barabara zinafika kila kijiji na kila kaya. Dada hao waliowahi kuthubutu kutumia kamba za kuteleza kwa elimu yao pia wamebadilisha maisha yao. Dada mkubwa amekuwa mfanyakazi wa afya wa kijiji, akilinda afya ya majirani zake, huku dada mdogo amegeukia kilimo cha mmea unaofanana na tangawizi, Caoguo, na hivyo kuongeza kipato chake katika safari ya kuelekea ustawi.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma