Kesi za Ebola nchini Kenya zafikia tisa

(CRI Online) Oktoba 21, 2026

Wizara ya Afya ya Kenya imesema, idadi ya kesi zilizothibitishwa za Ebola nchini humo imeongezeka na kufikia tisa, ikiwemo kifo cha mtu mmoja, na kwamba kesi zote zinatoka katika sehemu moja huku hakuna ushahidi wa maambukizi nje ya sehemu hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Afya katika Wizara hiyo, Patrick Amoth amesema, kesi ya tisa, iliyothibitishwa jumatatu wiki hii, ni kijana wa miaka 24 na mwanafamilia wa karibu wa kesi ya kwanza, na tayari alikuwa karantini alipoanza kuugua.

Amesema wagonjwa wote wanaendelea kupata huduma bora kutoka kwa timu za madaktari, na kwamba wanaendelea vizuri chini ya usimamizi wa karibu, na kuongeza kuwa, watu 134 kati ya 135 wamefuatiliwa na kutengwa mpaka kufikia jana jumanne.

Kenya ni nchi ya nne duniani kuthibitisha ugonjwa wa Ebola katika mlipuko wa sasa, kufuatia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Uganda, na Ufaransa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha