Lugha Nyingine
Rais wa Botswana asema uhusiano kati ya nchi yake na China umepanda ngazi na kuingia kipindi kipya cha urafiki wa kudumu
Rais wa Botswana Duma Gideon Boko amesema uhusiano kati ya nchi yake na China umepanda ngazi na kuwa uhusiano wa wenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote, na kuanza kipindi kipya cha urafiki wa kudumu.
Rais Boko amesema hayo baada ya kumaliza ziara yake ya kwanza ya kitaifa nchini China na kurudi Gaborone, mji mkuu wa Botswana.
Rais Boko amesema kupanda kwa ngazi ya uhusiano kati ya Botswana na China kumeweka msingi imara zaidi kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika sekta za biashara, madini, kilimo, afya, elimu, teknolojia ya kidijitali na miundo mbinu.
Pia ameongeza kuwa Botswana iko tayari kushirikiana na China katika kuoanisha mikakati ya maendeleo, na kwamba inakaribisha makampuni mengi zaidi ya China kuwekeza nchini Botswana.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma