Lugha Nyingine
Rais Xi apongeza maadhimisho ya miaka 70 tangu Taasisi Kuu ya Usoshalisti ianzishwe
Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Taasisi Kuu ya Usoshalisti, ikisherehekea maadhimisho yake ya miaka 70 tangu ianzishwe.
Katika barua hiyo, rais Xi ameipongeza taasisi hiyo kwa kutoa mafunzo kwa idadi kubwa ya wawakilishi wasio wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wanaochangia mawazo na kazi za Chama kuelekea malengo ya pamoja, na pia kwa mchango wake muhimu katika kuimarisha na kuendeleza umoja wa kizalendo katika miaka 70 iliyopita.
Ameitia moyo taasisi hiyo kuendelea kuimarisha mafunzo ya kisiasa, kujenga makubaliano mapana ya kisiasa, na kuimarisha ubora wa ufundishaji na utafiti wake pamoja na uwezo wake wa usimamizi.

Meli hospitali ya jeshi la majini la China yawasili Cote d'Ivoire kutekeleza jukumu la matibabu

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma