Mashambulizi ya droni yavuruga huduma muhimu nchini Sudan

(CRI Online) Oktoba 20, 2026

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yamesema yana wasiwasi na ripoti za kuendelea kwa mashambulizi mabaya ya droni nchini Sudan, ambayo yanasababisha vifo vya raia na kuvuruga huduma muhimu.

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, droni zimeripotiwa kushambulia maeneo katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum, ikiwemo karibu na uwanja wa ndege jana jumatatu, ambapo raia mmoja aliuawa na ndege kadhaa kusitisha safari zake.

OCHA imesema, shambulio la droni mkoani Darfur Magharibi jumamosi iliyopita lilisababisha vifo vya watu 11, wakiwemo watoto tisa, na kujeruhi wengine kadhaa katika eneo la Bir Saliba.

Katika mkoa wa Darfur Kusini, shambulio la droni lililotokea Ijumaa iliyopita katika soko la Almawashi katika mji mkuu wa mkoa huo, Nyala, lilisababisha vifo vya watu wasiopungua wanne, akiwemo mtoto mmoja.

Mkoani Kordofan Kaskazini, watu wanne waliuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la droni katika eneo la Abu Zabad jumamosi iliyopita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha