Taasisi za fedha barani Afrika zataka kuboresha miamala kwa kutumia sarafu ya China

(CRI Online) Oktoba 20, 2026

Serikali na taasisi za fedha barani Afrika zimekuwa zikiboresha hatua kwa hatua kukamilisha miamala ya kibiashara na kupanua matumizi ya sarafu ya China RMB, wakati China ikitekeleza kikamilifu sera ya ushuru sifuri kwa bidhaa zinazotoka nchi 53 za Afrika zenye uhusiano nayo wa kidiplomasia.

Kundi la Ecobank la nchini Togo, hivi karibuni limesaini Nyaraka ya Makubaliano (MoU) na Mfumo wa Malipo ya Kuvuka Mpaka kati ya Benki (CIPS) ili kuimarisha muungano wa malipo kwa kutumia RMB kati ya China na Afrika.

Benki ya Kigali nchini Rwanda, nayo imetangaza mwisho wa mwezi Septemba kwamba imeanza rasmi kuwa mshirika wa CIPS.

Tangu kuanza rasmi kwa utekelezaji wa sera ya ushuru sifuri ya China, thamani ya uagizaji wa bidhaa za Afrika nchini China imefikia dola za kimarekani bilioni 28.96 katika mwezi Mei na Juni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.5 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha