Msemaji: Kanuni 4 zilizopendekezwa na Rais wa China zina umuhimu wa kuelekeza katika kutatua masuala muhimu barani Afrika

(CRI Online) Oktoba 20, 2026

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, rais Xi Jinping wa China alipokutana na mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Togo Faure Essozimna Gnassingbé hivi karibuni hapa Beijing, alipendekeza kanuni 4 kwa pande husika kushiriki kwa njia ya kujenga kwenye utatuzi wa masuala muhimu ya Afrika.

Mao Ning alisema hayo alipoulizwa kama kanuni hizi zinahusika hali ya hivi sasa ya Kaskazini mwa Ethiopia au la, ambapo amesema, kanuni hizo zina umuhimu wa kuelekeza katika kutatua masuala muhimu katika bara la Afrika ikiwemo hali ya Pembe ya Afrika.

Amezitaja kanuni hizo kuwa ni kushikilia uongozi wa Afrika, kulinda haki na usawa, kusitisha uhasama kwa ajili ya amani, na kushughulikia dalili na vyanzo sababishi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha