Katika Kujenga Jamii Yenye Maisha Bora kwa pande zote, hakuna kabila hata moja linalopaswa kuachwa Nyuma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2026

Eneo la Nujiang linalojiendesha la Kabila la Walisu liko kaskazini-magharibi mwa Mkoa wa Yunnan, China, na linajumuisha mji wa Lushui, Wilaya ya Fugong, Wilaya ya Gongshan inayojiendesha ya Makabila ya Wadulong na Wanu, na Wilaya ya Lanping inayojiendesha ya Makabila ya Wabai na Wapumi. Katika eneo hilo wanaishi watu wa makabila 22, yakiwemo Walisu, Wanu, Wadulong na Wapumi, hali ambayo imelifanya liwe eneo linalojiendesha la watu wa makabila mengi zaidi nchini China, na pia ni eneo lenye makabila mengi zaidi yenye idadi ndogo ya watu.

Katika eneo hilo, ukubwa wa maeneo ya milima unachukua zaidi ya asilimia 98, na mandhari yake ya milima mirefu na mabonde makubwa inavutia sana. Hapo kabla, "Mto Nujiang unatiririka kila siku bila kusita, na kamba moja ya kuvuka mto inaunganisha pande zake mbili" ilikuwa hali halisi katika uzalishaji na maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Mwaka 2007, picha moja imeweka kumbukumbu za hali ngumu ya kuteleza kwenye kamba kwa kuvuka mto ili kwenda shuleni waliyoipita dada wawili wa kabila la Walisu, Yu Chunhua na Yu Caimei wa kijiji cha Majimi cha tarafa ya Maji katika wilaya ya Fugong.

Kutoka mwaka 2011 hadi 2016, Eneo la Nujiang likifuatiliwa na kuungwa mkono na serikali, lilianzisha kwa vipindi viwili ujenzi wa mradi wa "kujenga madaraja badala ya kamba" katika maeneo ya mito mitatu — Nujiang, Lancang na Dulongjiang, likijenga madaraja 36 kubadilisha jozi 42 za kamba zilizotumiwa kwa kuvuka mito, hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto za kuvuka mto kwa wakazi wa pande zote mbili za mito hiyo mitatu.

Tarehe 30 Desemba 2018, chini ya msaada wa Kundi la Gazeti la Yunnan Daily, daraja la Qiaoma la kuvuka mto lilikamilika baada ya kujengwa kwa zaidi ya miezi tisa, na kuondoa kabisa tatizo la kuvuka mto kwa wakazi wa kikundi cha Qiaomaga katika kijiji cha Majimi.

"Sasa tumekuwa na daraja, kwa hivyo hatuhitaji tena kuvuka mto kwa kuteleza kwenye kamba. Katika miaka hii, mabadiliko makubwa yametokea katika maisha yetu,” Yu Chunhua alisema kwa msisimko.

Mpaka hivi sasa, katika tarafa ya Maji madaraja 16 ya kuvuka mto yamejengwa tayari, na barabara hizo zimepita vijijini na kuunganisha nyumbani kwa wakazi. Dada Yu Chunhua amekuwa mhudumu wa afya wa vijijini; Dada Yu Caimei alirejea kijijini kupanda mimea ya iliki aina ya "Caoguo," na anaweza kusaidia familia yake kuongeza kipato kwa yuan 20,000 hivi kila mwaka.

Tarafa ya Dulongjiang katika Wilaya ya Gongshan ni eneo muhimu wanapoishi watu wa kabila la Wadulong, na idadi ya watu wa kabila hilo ni ndogo. Kutokana na vizuizi vya mazingira ya asili na sababu nyinginezo, eneo hilo lilikuwa moja ya maeneo yenye umaskini zaidi na yaliyopo nyuma zaidi kimaendeleo mkoani Yunnan na hata nchini China.

Mwanzoni mwa mwaka 2014, Katibu Mkuu Xi Jinping alitoa maagizo muhimu kuhusu handaki la barabara la Dulongjiang Mlimani Galigong lililopo kwenye Tarafa ya Dulongjiang ya Wilaya ya Gongshan, ambalo lilikuwa karibu kukamilika, na aliwatia moyo Wadulong “kujiendeleza kwa haraka ili kuondokana na umaskini na kupata utajiri, na mapema iwezekanavyo kuishi maisha bora pamoja na watu wa makabila mengine nchini kote”; Mwezi Aprili, handaki la barabara la Dulongjiang lilikamilika kwa mafanikio, kuanzia hapo, siku zile za kufungwa kwa nusu mwaka kwenye maeneo ya milima kutokana na theluji kubwa zimekuwa historia kabisa kwa Wadulong.

Tarehe 20 Januari 2015, Katibu Mkuu Xi Jinping alipokutana na wajumbe wa makada na wakazi wa wilaya ya Gongshan huko Kunming, Yunnan, alisema: "Katika kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote, hakuna kabila hata moja litakaloachwa nyuma." Mwishoni mwa mwaka 2018, Wadulong wote waliondokana na umaskini, wakifikia mabadiliko ya kihistoria kutoka umaskini hadi jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

Mwezi Mei 2022, baada ya kuzinduliwa kwa mradi wa kuunganisha gridi wa kilovolt 35 wa Gridi ya Umeme ya Kusini ya China katika tarafa ya Dulongjiang, tarafa hiyo iliagana na historia ya utumiaji wa umeme usio wa tulivu. Hivi sasa, nyumba za wakazi za kuwapokea watalii na hoteli ndogo za eneo hilo zimeongezeka kwa haraka, na mahitaji ya umeme yanayoongezeka mwaka hadi mwaka ni ushahidi mzuri kwa maisha ya wakazi yanayozidi kuwa na urahisi na njia zao za uzalishaji zinaendelea kuboreshwa.

Blanketi za Wadulong ni bidhaa za mikono zenye sifa maalum zaidi za kabila la Wadulong. Mkazi wa kijiji cha Dizhengdang, Li Yuhua, alianzisha Ushirika wa kusuka na kutengeneza blanketi za Wadulong, akiwaongoza madada wa kijijini hapo kurithisha ufundi huu wa kijadi na kuhuisha kazi za kutengeneza bidhaa za ubunifu wa kitamaduni kama vile skafu na mifuko ya kubebea, ambazo watalii wanazipenda sana.

“Kuondokana na umaskini ni kupiga hatua ya kwanza tu, siku bora zaidi bado zinakuja.” Mwezi Aprili 2019, Katibu Mkuu Xi Jinping aliwajibu barua ya wakazi wa tarafa ya Dulongjiang, akiwapongeza Wadulong wote kwa kuondokana na umaskini, na kuwatia moyo kuendelea na mshikamano na kufanya juhudi zaidi kwa ajili ya kuishi maisha mazuri yenye furaha zaidi. He Shancong, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Utoaji wa Umeme ya Gongshan ya Gridi ya Kusini ya China alisema, kwa kutiwa moyo na barua ya Katibu Mkuu Xi, watashirikiana kwa moyo mmoja katika kujenga vizuri nyumbani kwao na kulinda mipaka ya nchi, na kujenga siku nzuri zaidi za baadaye kwa mikono yao yenye bidii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha