Barabara Inayoelekea Maisha Bora

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 19, 2026

"Ukitaka kutajirika, jenga barabara kwanza.” Usemi huu ambao Wachina wengi wanaifahamu vizuri, sasa unapata mwitikio mpya katika bara la Afrika.

Kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi, hadi mji mkubwa wa viwanda, Thika, barabara ya awali ilikumbwa na msongamano mkubwa, na wakati wa asubuhi na jioni wa kilele cha msongamano, usafiri wa kupita njia nzima ulichukua muda wa saa mbili. Kuanzia mwaka 2009, makampuni matatu ya China yaliyokabidhiwa kazi za ukarabati na upanuzi wa sehemu tofauti za barabara hiyo, na yalifanya barabara hiyo yenye njia nne (njia mbili kwa kila upande) kuwa ya njia sita au nane (njia tatu au nne kwa kila upande), hivyo mawasiliano kati ya Nairobi na Thika yamekuwa ya karibu zaidi.

Baada ya barabara kuu ya Thika kuanza kutumika, muda wa usafiri wa kupita njia nzima ulipungua kuwa dakika 30 au 40 hivi. Kwa sasa zaidi ya miaka kumi imepita, na barabara hii muhimu ya usafiri bado ina mtiririko usiokoma wa magari, ikiendelea kuwahudumia wakazi wa sehemu za kando mbili za barabara na maendeleo ya uchumi wa kikanda.

Hali inayobadilika kutokana na barabara siyo muda wa usafiri tu. Bidhaa zinaweza kuingia sokoni kwa haraka zaidi, usafiri wa watu umekuwa na urahisi zaidi, na makazi, biashara pamoja na shughuli za viwanda kando za barabara vinaendelezwa kutokana na ujenzi wa barabara; Barabara inayoelekea kaskazini pia imeleta mazingira bora zaidi kwa mawasiliano ya kibiashara na ya kiuchumi kati ya Kenya na nchi jirani Ethiopia na nyinginezo.

Mshipa mwingine wa uchumi unaboreshwa nchini Afrika Kusini. Barabara ya N3 inayounganisha Johannesburg na Bandari ya Durban ni njia muhimu ya usafirishaji wa bidhaa nchini Afrika Kusini na hata ukanda wa kusini mwa Afrika. Kampuni ya Ujenzi ya China (China State Construction) na makampuni ya Afrika Kusini yaliunda muungano wa uendeshaji, na kubeba kazi za ukarabati na upanuzi wa sehemu ya barabara ya N3 pamoja na makutano ya N2 na N3, ili kuongeza uwezo wa usafiri kwenye barabara hiyo yenye msongamano.

Barabara inaunganisha bandari na miji, bidhaa na masoko, na pia imeleta utoaji wa mafunzo ya kazi za ufundi na fursa za ajira. Mradi wa ukarabati na upanuzi wa barabara ya N3 ulitoa nafasi za ajira kwa wafanyakazi 520 hivi, na umesaidia kuwaandaa vijana 200 na zaidi wa eneo hilo. Wajenzi kutoka nchi mbalimbali wamepitia hatua ya mwanzo ya kuzoeana na kufikia hali ya kuaminiana na kufanya kazi kwa ushirikiano. Kama alivyosema mmoja wa meneja wa ujenzi wa Afrika Kusini: "Sasa tuko kama ndugu."

Tarehe 5 Septemba 2024, Rais Xi Jinping alipotoa hotuba yake kuu kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, alitangaza kwamba katika miaka mitatu ijayo, China inapenda kushirikiana na Afrika katika kutekeleza “Hatua Kumi za Ushirikiano” za China na Afrika kuendeleza kwa pamoja mambo ya kisasa, kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuongoza maendeleo ya mambo ya kisasa ya Kusini mwa Dunia.

Kutoka barabara kuu ya Thika nchini Kenya iliyotumika kwa zaidi ya miaka kumi, hadi mradi wa ukarabati na upanuzi wa N3 nchini Afrika Kusini unaoendelea, ushirikiano kati ya China na Afrika unaendelea kutoka ujenzi wa miundombinu hadi utoaji mafunzo ya kazi za ufundi, utoaji wa nafasi za ajira na maendeleo ya maeneo ya makazi. Kutoka uzoefu wa China hadi utekelezaji wake barani Afrika, uzoefu wa China wa kupunguza umaskini unabadilika kuwa matokeo ya maendeleo kwa kufuata hali halisi ya eneo husika, ukifungua fursa zaidi kwa Kusini mwa Dunia kuelekea mambo ya kisasa, na kutandaza barabara isiyo na umaskini wala mwisho, ambayo inaunganisha fursa, ongezeko na matumaini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha