Mlipuko wa Ebola waenea katika mkoa wa nane nchini DRC

(CRI Online) Oktoba 19, 2026

Mlipuko unaoendelea wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) umeenea katika mkoa wa nane, huku kesi mpya zikithibitishwa katika mkoa wa Nord-Ubangi, kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana jumapili na Wizara ya Afya nchini humo, wanaume wawili wameripotiwa kuwa na maambukizi katika ukanda wa afya wa Wapinda, na mmoja kati yao amefariki.

Mpaka kufikia ijumaa iliyopita, DRC imerekodi kesi 9,415 zilizothibitishwa, ikiwemo vifo 4,536, tangu mlipuko huo ulipotokea mwezi Mei. Mkoa wa Ituri mashariki mwa nchi hiyo umedumu kuwa kitovu cha mlipuko, ukiwa na zaidi ya asilimia 73 ya kesi zote zilizothibitishwa nchini humo, ukifuatiwa na mkoa wa Kivu Kaskazini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha