Lugha Nyingine
Mkutano wa 17 wa Washiriki wa Mkataba wa Bioanuwai wakagua maendeleo ya utekelezaji wa malengo ya kimataifa
![]() |
| (Picha/Xinhua) |
Mkutano wa 17 wa Watia saini wa Mkataba wa Anuwai ya Kibiolojia (COP17) unafanyika kuanzia tarehe 19 hadi 30 mwezi huu katika mji mkuu wa Armenia, Yerevan.
Mkutano huu utakagua utekelezaji wa “Mfumo wa Kimataifa wa Bioanuwai wa Kunming-Montreal”. Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba huo, Bi. Astrid Schomaker, alipohojiwa na mwanahabari wa CMG, alisema inatarajiwa kwamba Washiriki watafikia maamuzi 54 katika kipindi cha takriban siku 10.
Mwaka 2022, Mkutano wa 15 wa Watia saini wa Mkataba huo ulipitisha “Mfumo wa Bioanuwaiwa Kunming-Montreal”, ukiweka malengo 23 ya kivitendo ya kimataifa kufikia mwaka 2030, kwa ajili ya kuzuia na kubadilisha upotevu wa mazingira ya asili. Bi. Schomaker alinukuu ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa tarehe 15 iitwayo “Hali ya Utekelezaji kuhusu Anuwai ya Kibiolojia”, akisema ingawa nchi zimechukua hatua kuhusu malengo yote 23, maendeleo kwa sasa si ya kuridhisha. Kwa hivyomkutano wa awamu hiiunatakiwa kujadili jinsi pande mbalimbali husika zinavyoweza kushauriana.

Tamasha la 19 la Utamaduni na Utalii la A-Ma lafunguliwa Macao, China

Utandazaji wa reli waanza kwenye reli ya mwendo-kasi ya Nantong-Ningbo mkoani Jiangsu, China

Mabaki ya vivutio vya kihistoria vya Safari Ndefu mkoani Sichuan, China

Mwonekano wa kisiwa cha Liugong la eneo la mji Weihai mkoani Shandong China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
