Lugha Nyingine
Kanuni za Xi juu ya kutatua masuala ya migogoro barani Afrika zaungwa mkono kote barani

Picha hii iliyopigwa Januari 23, 2025, ikionesha treni zikisubiri matengenezo nje ya karakana ya Reli ya Mombasa-Nairobi jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Wang Guansen)
NAIROBI - Kanuni nne zilizopendekezwa na Rais wa China Xi Jinping kwa ajili ya kutatua masuala ya migogoro barani Afrika zimepokelewa vyema kote barani humo huku wanadiplomasia, wasomi, na wataalamu wa vyombo vya habari wakizisifu kwa kuzielezea kuwa ni mwongozo uliokuja katika wakati muafaka na wa kivitendo katika kuhimiza amani na maendeleo barani Afrika.
Kanuni hizo nne — kutilia maanani misingi ya "Afrika kuongoza," kushikilia haki na usawa, kuhimiza kusitisha uhasama kwa ajili ya amani, na kushughulikia dalili na vyanzo sababishi — zilitolewa Jumanne wiki hii mjini Beijing kwenye mkutano kati ya Xi na Faure Essozimna Gnassingbe, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Togo, ambaye alikuwa katika ziara rasmi nchini China.
Wakibainisha kuwa pendekezo hilo limekuja wakati ambapo migogoro barani humo inazidishwa na uingiliaji wa nje pamoja na ushindani unaozidi kuongezeka wa siasa za kijiografia, wataalam hao wa Afrika wamesema wanaunga mkono msisitizo wake katika kujenga usalama wa kudumu kupitia umiliki wa Afrika yenyewe, usawa wa kimataifa, majadiliano ya amani, na maendeleo endelevu.
Akizungumzia juu ya umiliki wa Afrika kwa mambo yake, Claudio Rabenja, mchumi kutoka Madagascar na mtaalamu wa masuala ya kimataifa, amesema kanuni hiyo "ni yenye mantiki na ni muhimu sana katika muktadha wa sasa wa siasa za kijiografia, “kwani migogoro barani Afrika inatokana na mambo tata ya ndani ambayo mara nyingi wahusika wa nje hushindwa kuyaelewa.

Ndege inayoendeshwa na shirika la ndege la China Southern ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Addis Ababa Bole mjini Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Oktoba 12, 2026. (Xinhua/Geng Xinning)
Juu ya kanuni ya haki na usawa, Gerard Njoya, mhariri mkuu wa Actu Chine Cameroon, amesema kanuni hiyo inaimarisha Ajenda 2063 ya Umoja wa Afrika (AU) kwa kupinga vikwazo vya upande mmoja na uingiliaji kati usio na msingi, na kushughulikia hitaji la muda mrefu la "kukomesha uingiliaji kati wa nje na viwango viwili."
Kuhusu kanuni ya kutimiza amani kupitia mazungumzo, wataalamu hao huku wakibainisha kuwa vita na vikwazo vya upande mmoja haviwezi kimsingi kutatua migogoro, wamesema kanuni ya kuhimiza amani kupitia kusitisha uhasama inatoa wito wa kuheshimiana, mashauriano ya kina, kutafuta mwafaka wa pamoja wakati huohuo kuweka pembeni tofauti, na kujenga uelewa wa pamoja na kufaana.
Moutlakgola Masire, mwandishi wa habari katika Radio Botswana, amesema mashauriano yanayohusisha wadau mbalimbali na ahadi za kusimamisha mapigano zinaweza kuzuia mateso zaidi kwa raia na kufungua njia kwa ajili ya suluhu endelevu.

Mhandisi wa mawasiliano Zhou Junbing (kulia) akizungumza na dereva wa treni Mkenya ndani ya treni inayoelekea Mombasa kwenye Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi, nchini Kenya, Julai 23, 2026. (Xinhua/Yang Guang)
Kwa kuwa kanuni ya kushughulikia dalili na vyanzo sababishi inatoa wito wa kukabiliana na vitisho vya usalama vya haraka wakati huohuo kutafuta maendeleo ya muda mrefu, wataalamu hao wamesema China inaweza kuisaidia Afrika kukabiliana na changamoto zake, wakitolea mfano mchango wake katika ujenzi wa miundombinu, ufadhili wa masomo, na mafunzo ya ufundi kote barani humo.
Rabenja ameuelezea usalama na maendeleo kuwa ni "pande mbili za utulivu ambazo haziwezi kutenganishwa."
Mbali na kulinda raia kwa muda mfupi, amesema vyanzo vya msingi vya migogoro—kama vile umaskini, ukosefu wa ajira kwa vijana, ukosefu wa usawa, na taasisi dhaifu—lazima vishughulikiwe kupitia uwekezaji katika elimu, kilimo, nishati, miundombinu, na viwanda.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



