Rais Xi atuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya 140 ya Canton

(CRI Online) Oktoba 15, 2026

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya 140 ya uagizaji na uuzaji nje bidhaa ya China, Canton Fair.

Rais Xi amesema, tangu maonesho ya Canton Fair yaanzishwe miaka 70 iliyopita, yametoa mchango muhimu katika mawasiliano ya kibiashara kati ya China na nchi za nje, yakiwa ni jukwaa lenye ufanisi ambalo China inaongeza kiwango cha ufunguaji mlango na kuhimiza ujenzi wa uchumi wa dunia ulio wazi.

Rais Xi amesema katika hali mpya, China inapenda kushikana mkono na nchi mbalimbali duniani, ili kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi, kuhakikisha utulivu wa mnyororo wa utoaji na mnyororo wa viwanda duniani, kupanua nafasi za ushirikiano wa kunufaishana wa uchumi na biashara za kimataifa, kuhimiza mafungamano ya uchumi yaliyo jumuishi na kutia nguvu mpya katika ustawi na maendeleo ya dunia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha