Ni simulizi zipi zinafichwa katika kazi hii ya kudarizi ya Enzi ya Qing?

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 14, 2026

Nani anasema kazi ya kudarizi ya wakati wa kale haiwezi kuonekana mpya? Katika Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Qiandongnan, Mkoa wa Guizhou kusini-magharibi mwa China, mafundi mahiri wanasanifu upya udarizi wa kabila la Washui wa kutumia nywele za mkia wa farasi kwenye vibebea watoto vya Enzi ya Qing (1644-1911), na kuudarizi kwenye mikoba ya kimitindo. Mbinu hii ya "udarizi wa zamani, maisha mapya" inaupa ufundi huu wenye umri wa karne kadhaa mwanzo kabisa wa uhai mpya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha