Lugha Nyingine
Mabadiliko ya Mji wa Theluji: Namna barafu na theluji vilivyoinua 'ustawi' wa ardhi ya udongo mweusi
Utalii wa barafu na theluji unahuisha rasilimali za eneo husika. Tamaduni za makabila zinajitokeza dhahiri kutoka milimani. Usimamizi wa ikolojia unafanya ardhi kuwa mpya.
"Mfuate Xi," safu maalum ya video ya People's Daily Online, imezindua mfululizo wa video zenye kichwa "Jibu la China katika Kupunguza Umaskini Duniani," zikielezea juhudi za China za kupunguza umaskini kupitia maendeleo—zilizoandaliwa mahsusi kulingana na hali halisi ya kila eneo. Mabadiliko katika maisha ya watu wa kawaida ndiyo ushahidi thabiti zaidi. Hatua hizi za China pia zinatoa mafunzo kwa upunguzaji umaskini duniani.
Shamba la Misitu la Shuangfeng katika Mji wa Mudanjiang, Mkoa wa Heilongjiang kaskazini-mashariki mwa China, linajulikana kwa kuanguka kwa wingi kwa theluji; huku msimu wa theluji ukidumu kwa kipindi cha hadi miezi saba na kiasi cha mkusanyiko wa theluji kinaweza kufikia kina cha mita mbili.
Zhang Wei, awali alikuwa mfanyakazi wa kawaida kwenye Shamba hilo la Misitu la Shuangfeng. Siku za nyuma, theluji ilifika kiunoni mwake, na ilimbidi kutumia vyote mikono na miguu yake kupita kwenye njia za msituni—hii ilikuwa ni ratiba yake ya kila siku wakati wa majira ya baridi. Wakati huo, baridi kali na theluji nyingi vilikuwa ni changamoto kubwa, lakini pia vilikuwa alama ya miaka ya juhudi nyingi zaidi kwa wafanyakazi katika maeneo ya misituni kaskazini-mashariki mwa China.
Katika miaka ya 1980, mandhari ya kipekee ya theluji katika Shamba la Misitu la Shuangfeng ilipigwa picha mbalimbali, na jina la "Mji wa Theluji” lilianza kusambaa zaidi ya eneo hilo.
Mwaka 2014, shughuli za kibiashara za ukataji miti zilisimamishwa ili kulinda mfumo wa ikolojia. Wafanyakazi wa misitu waliokuwa wakitegemea ukataji miti walikabiliwa na changamoto ya kubadili njia zao za kujipatia kipato. Zhang alibadilika kutoka kuwa mfanyakazi wa misitu hadi kuwa mfanyakazi katika "Mji wa Theluji," akishiriki katika uundaji wa sanamu za barafu na theluji, mapambo ya gwaride, na usimamizi wa usalama katika maeneo ya vivutio vya watalii, akigeuza rasilimali za barafu na theluji kuwa kichocheo kipya cha utalii wa ikolojia. Mikono yake ilichonga barafu na theluji, lakini pia ilichonga ukurasa mpya katika maisha yake mwenyewe.
Waendeshaji wa zamani wa matrekta ya misituni, waendeshaji misumeno ya mnyororo na madereva wa kusafirisha mbao wote wamepata majukumu mapya katika tasnia ya barafu na theluji: Baadhi wamefungua nyumba za wageni za familia, wengine wanaendesha magari ya kufanyia utalii wa kutazama mandhari. Uchumi wa barafu na theluji umekuwa injini mpya ya ustawi wa wenyeji.
Leo hii, Mji huo wa Theluji ni nyumbani kwa kampuni zaidi ya 200, hupokea watalii zaidi ya 800,000 kila msimu wa baridi, hutoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya 1,000 wa zamani wa misitu na ina watu zaidi ya 5,500 walioajiriwa katika eneo hilo la kivutio cha watalii. Barafu na theluji si tu vinaangaza mafungamano ya utamaduni na utalii lakini pia vinachochea uboreshaji wa kiviwanda, vikitumika kama nguzo muhimu ya ustawishaji wa vijijini kaskazini mashariki mwa China.
Kama Rais wa China Xi Jinping alivyosema, "Barafu na theluji vimekuwa mali muhimu kwa watu kupata utajiri na kwa ajili ya ustawishaji wa vijijini." Mabadiliko makubwa ya Mji wa Theluji ni mfano dhahiri wa upunguzaji umaskini wa China unaolinda uoto wa kijani katika vitendo: kutumia ipasavyo maliasili, kutoa kipaumbele kwa ulinzi wa ikolojia na kubadilisha uzuri wa mandhari kuwa njia bora ya kujipatia riziki. Uzoefu huu unafaidisha jamii za wenyeji na unaonesha kwa dunia mbinu ya China ya kuchanganya maendeleo ya kijani, ustawishaji wa vijijini na upunguzaji umaskini.
Baridi kali na theluji nyingi vimekuwa mali za thamani kwa ukuaji wa uchumi. Kwa jasho na werevu, Zhang na wenzake wamegeuza "bakuli la mbao" la msituni kuwa "bonde la hazina," wakiwezesha udongo mweusi kukusanya nguvu katika barafu na theluji, hivyo kukaribisha chemchemi iliyojaa matumaini na kuandika ukurasa duniani katika simulizi ya kupunguza umaskini ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



