Rais wa Botswana asema Botswana inalenga kuimarisha na kuzidisha uhusiano na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2026

Rais wa Botswana, Duma Gideon Boko, akizungumza kwenye mahojiano maalum na shirika la habari la China, Xinhua jijini Gaborone, Botswana, tarehe 9 Oktoba 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Rais wa Botswana, Duma Gideon Boko, akizungumza kwenye mahojiano maalum na shirika la habari la China, Xinhua jijini Gaborone, Botswana, tarehe 9 Oktoba 2026. (Xinhua/Chen Wei)

GABORONE - Rais wa Botswana, Duma Gideon Boko amesema uhusiano kati ya Botswana na China ni "wa kina na imara," na Botswana inatarajia kuongeza zaidi ushirikiano wa pande mbili katika sekta za biashara, uchumi wa kidijitali, na nishati mbadala.

Katika mahojiano na shirika la habari la China, Xinhua ya hivi karibuni kabla ya ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini China tangu alipoingia madarakani, Boko amesema kuwa pande hizo mbili zinadumisha "uhusiano mzuri sana wa kidiplomasia ulio wa imara sana, na wa kunufaishana" kwa miaka mingi.

Rais huyo amesema, "katika miaka mingi iliyopita, China imetoa msaada mkubwa kwa maendeleo ya Jamhuri ya Botswana," na Botswana pia inatarajia kunufaika na utaalamu wa teknolojia wa China, ukiwemo ule wa kampuni ambazo tayari zinaendesha shughuli zake nchini Botswana.

"Tunatarajia kupanua na kuzidisha uwepo huo, na kualika kampuni nyingine zitakazoshiriki katika miradi mikubwa nchini Botswana," amesema.

“Botswana pia inatumai kuzidisha uhusiano wa kibiashara na China kwa njia nyingine ikiwemo kushirikiana na kampuni za China ambazo zimewekeza kwa kiasi kikubwa katika utafiti na maendeleo yanayohusiana na nyongeza za thamani," Boko amesema, akiongeza kuwa hatua hiyo "itawezesha Botswana kuwa mzalishaji, hivyo, itaweza kutoa huduma nzuri zaidi kwenye soko la China."

Kuanzia tarehe 1 Mei mwaka huu, China ilipanua utaratibu wa kutoza ushuru-sifuri wa forodha kwa nchi zote 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China. Boko amesema, hii ni "hatua ya serikali ya China inayokabishwa sana na kustahili kusifiwa sana," na hatua hiyo imefungua "soko lenye watumizi bilioni 1.4 kwa ajili ya mazao na bidhaa za Afrika."

"Hii inafanya uhusiano wa kibiashara kati ya Afrika na China iendelee vizuri zaidi, na itasaidia uchumi wetu," amesema, "Lakini muhimu zaidi, kwa upande wa Botswana, tutasaini makubaliano ambayo yatawezesha mazao yetu ya matunda jamii ya machungwa kuingia China chini ya utaratibu wa bila-ushuru, jambo ambalo ni faida kubwa sana kwa nchi yetu."

Kuhusu mambo ya kidijitali na uchumi wa aina mbalimbali, Rais Boko amesema kuwa Botswana inatarajia kunufaika na utaalamu wa China. "China ina uwezo, nguvu na uwezekano... kuleta huo uwezekano nchini Botswana kwa maendeleo ya uchumi wa Botswana, na uchumi wa ukanda wa SADC (Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika) na bara la Afrika," amesema.

Rais huyo wa Botswana pia amesema kuwa uzoefu wa China katika maendeleo ya nishati mbadala, uhifadhi wa nishati, miundombinu ya umeme na viwanda vingine vya kijani ndiyo hasa ambao Botswana inahitaji, na akiongeza kuwa nchi yake imefungua milango kwa wafanyabiashara wa China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha