Lugha Nyingine
Iran yasema iko tayari kusaidia kuanzisha mazungumzo kati ya Saudi Arabia na Yemen
(CRI Online) Oktoba 12, 2026
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema nchi yake iko tayari kutoa msaada wa aina yoyote ili kusaidia kuanzisha mazungumzo kati ya Saudi Arabia na Yemen na kuandaa mazingira ya kufikia suluhu ya kisiasa kwa mgogoro unaoendelea.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Araghchi alifanya mazungumzo ya simu na mwenzake wa Saudi Arabia, Mwanamfalme Faisal bin Farhan bin Abdullah Al Saud, ambapo pande hizo mbili zilijadili hali inayoendelea katika eneo la Asia Magharibi.
Araghchi ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa mivutano, akisema kuwa kung’ang’ania kutumia njia za kijeshi na kupuuza suluhu za kisiasa kunafanya hali kuwa mbaya zaidi. Amesisitiza kuwa hakuna suluhu ya kijeshi kwa migogoro ya Asia Magharibi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



