Uingereza haiungi mkono makubaliano ya Trump na Russia kuhusu dizeli: Waziri wa Ulinzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 12, 2026

Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2026 ikionesha Wizara ya Ulinzi ya Uingereza jijini London, Uingereza. (Xinhua/Zhang Feng)

Picha iliyopigwa Oktoba 11, 2026 ikionesha Wizara ya Ulinzi ya Uingereza jijini London, Uingereza. (Xinhua/Zhang Feng)

LONDON - Uingereza haiungi mkono makubaliano kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Russia Vladimir Putin ya kununua mamilioni ya tani za dizeli kutoka Russia, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Wes Streeting amesema jana Jumapili.

"Hatuungi mkono uamuzi huo. Kama Waziri Mkuu alivyoeleza wazi, tunaimarisha vikwazo dhidi ya Russia," Streeting amesema katika mahojiano yaliyorushwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Ameongeza kuwa makubaliano hayo yamefikiwa "kwa kiasi kikubwa katika muktadha wa uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani" mwezi Novemba, wakati ambapo wanasiasa kote duniani wako katika shinikizo la kupunguza gharama za maisha.

Makubaliano hayo ya dizeli ya Trump yanalenga kushusha bei ya mafuta nchini Marekani, ambayo imepanda kufuatia mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, kwa mujibu wa ripoti ya BBC.

Siku ya Ijumaa, Washington ilitangaza hatua za kupunguza vikwazo dhidi ya biashara ya dizeli ya Russia. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekosoa hatua hiyo, akisema kuwa kuiruhusu Russia kuuza bidhaa za mafuta ni sawa na kuwekeza kwenye vita.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha