Bibi wa kabila la Wamiao la China abeba sanaa ya kudarizi ya Wamiao kwenye jukwaa la dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 10, 2026

Kutoka kwenye duka dogo la sanaa ya kudarizi ya kabila la Wamiao milimani nchini China hadi kwenye jukwaa la maonyesho ya wiki ya mitindo ya kimataifa, Bibi Li anaipeleka sanaa hiyo ya nyumbani kwao duniani kote. Akitokea Kaili, katika Mkoa wa Guizhou kusini-magharibi mwa China, amepanda jukwaa la dunia akiwa amevalia vazi la kabila la Wamiao aliloshona kwa mikono yake mwenyewe, akibeba simulizi za nyumbani ambako ni chimbuko lake mbali zaidi ya milima hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha