Mke wa Rais wa China Peng Liyuan atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusukuma mbele elimu ya wanawake

(CRI Online) Oktoba 10, 2026

Peng Liyuan, mke wa rais wa China ambaye pia ni mjumbe maalum wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) kwa ajili ya kusukuma mbele elimu ya wasichana na wanawake, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza kwa nguvu elimu ya mambo ya kidigitali na AI kwa wanawake, ili kuhakikisha kwamba wanaweza kutumia na kunufaika na teknolojia za kidigitali na AI.

Bi. Peng ametoa wito huo kwa njia ya video kwenye hafla ya Tuzo ya UNESCO ya Elimu kwa Wasichana na Wanawake ya 2026, iliyofanyika jana Ijumaa mjini Paris.

Huku akieleza kuwa elimu ya wasichana na wanawake bado ni jukumu gumu, Bi. Peng ameihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja ili kuboresha elimu ya ufundi stadi na mafunzo ya wanawake na kuwajengea ngazi ya kufikia maisha yenye ubora.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha