Lugha Nyingine
Benki Kuu ya Tanzania yasema Uchumi wa Tanzania umedumisha kasi imara ya ukuaji mwaka 2026
imara ya ukuaji katika mwaka huu, huku uchumi wa Tanzania Bara ukiongezeka kwa asilimia 6 katika robo ya kwanza na unakadiriwa kukua kwa asilimia zaidi ya 6 katika robo ya pili na ya tatu.
Katika taarifa yake jana Alhamisi jijini Dar es Salaam, Bw. Tutuba amesema huduma za kifedha, uzalishaji wa viwandani, uwekezaji katika miundombinu na huduma za kijamii vimechangia ukuaji huo.
Amesema uchumi wa Zanzibar ulikua kwa asilimia 6.7 katika robo ya kwanza na unakadiriwa kukua kwa asilimia zaidi ya 7 katika robo ya pili na ya tatu, ukichochewa na sekta za utalii, ujenzi na miradi ya umwagiliaji.
Bw. Tutuba amesema kuwa zoezi la hivi punde zaidi la mapitio ya msingi wa hesabu za Pato la Taifa (GDP) limeongeza hesabu za GDP ya Tanzania Bara katika mwaka 2025 hadi shilingi trilioni 234.104 (dola takribani bilioni 92.3 za Marekani) kutoka shilingi trilioni 230.073 ya mwaka uliotangulia wa 2024. Amesema, GDP ya Zanzibar iliongezeka kutoka Shilingi trilioni 7.029 hadi trilioni 9.242.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



