Lugha Nyingine
China yatoa msaada wa dola milioni 2 kwa Kenya kwa ajili ya kujiandaa kwa Ebola na misaada ya ukame
Kenya imepokea msaada wa fedha taslimu wa jumla ya dola milioni 2 za kimarekani kutoka kwa China ili kuunga mkono mapambano yake dhidi ya Ebola na misaada ya kukabiliana na ukame.
Balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan, Katibu Mkuu wa Hazina ya Kenya Bw. Chris Kiptoo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Umma ya Kenya Bi. Mary Muthoni walihudhuria hafla ya makabidhiano iliyofanyika jana Alhamisi mjini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambapo pande hizo mbili zilisaini hati ya makabidhiano.
Msaada huo umetokana na majibu kwa ombi kutoka kwa serikali ya Kenya, ambapo dola milioni 1 zitatumika kuimarisha miundombinu kwa ajili ya kujiandaa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa kaunti zilizobainisha kuwa hatarini sana na hatarini, na nyingine milioni 1 zitatumika kuunga mkono mwitikio wa serikali ya Kenya katika athari za ukame.
Balozi Guo amesisitiza kuwa msaada huo kwa Kenya unaonesha hisia ya kirafiki inayobebwa na serikali ya China na watu wake kwa serikali na watu wa Jamhuri ya Kenya.
Balozi huyo ameeleza nia ya China ya kuendelea kuimarisha ushirikiano wa maendeleo na Kenya chini ya mifumo ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) na Pendekezo la Maendeleo ya Dunia (GDl).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



