Rais wa Kenya aagiza kuongeza hatua za dharura baada ya kubainika kwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola

(CRI Online) Oktoba 08, 2026

Rais William Ruto wa Kenya ameagiza mamlaka za afya kuongeza hatua za dharura kufuatia kifo cha mgonjwa aliyethibitishwa kuwa wa kwanza wa nchi hiyo kuambukizwa virusi vya Ebola ya Bundibugyo (BVD) kutokea nje ya Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumatano jioni, Rais Ruto ameiagiza Kamati ya Baraza la Usalama wa Taifa kukutana, kufanya tathmini ya hali na kupendekeza hatua za kulinda taifa.

Amesema serikali imeongeza ufuatiliaji, utafutaji wa watu waliokutana kwa karibu na mgonjwa na hatua za afya ya umma ili kuzuia uwezekano wa kutokea kwa maambukizi ya virusi hivyo, huku wanafamilia wanane wa mgonjwa huyo aliyefariki wakiwekwa karantini na kufanyiwa ufuatiliaji wa dalili wa kila siku.

Wakati huohuo, Sudan Kusini imeimarisha maandalizi na usimamizi wa taifa dhidi ya ugonjwa huo wa BVD baada ya kubainika kwa mgonjwa huyo nchini Kenya. Wizara ya Afya ya nchi hiyo imesema hakuna mtu aliyethibitishwa kuambukizwa nchini humo, na kwamba mfumo wa afya umewekwa katika hali ya tahadhari ya kiwango cha juu.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha