Lugha Nyingine
China yaihimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuchangia amani na maendeleo ya nchi za Afrika
Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuchangia amani na maendeleo ya nchi za Afrika.
Balozi Fu ameyasema hayo kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu “Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika”. Amesema, Afrika inakuwa ncha muhimu yenye ushawishi kwa dunia nzima. Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ukiwa ni mfano wa ushirikiano wa pande nyingi, umefanya kazi muhimu katika kuhimiza amani, utulivu na maendeleo barani Afrika.
Balozi Fu ametoa mapendekezo matatu kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia amani na maendeleo ya Afrika. Kwanza ni kuhimiza masuala nyeti kutatuliwa kwa njia ya kisiasa, na kujenga kwa pamoja amani na utulivu barani Afrika. Pili ni kuongeza uwekezaji kwa maendeleo ya Afrika, na kuchangia ustawi wa bara hilo. Tatu ni kuendeleza mageuzi na kuboresha usimamizi wa dunia, na kuiunga mkono Afrika kujitegemea na kujiendeleza.
Balozi Fu amesisitiza kuwa mwaka huu ni wa 70 tangu China na nchi za Afrika zianzishe rasmi uhusiano wa kidiplomasia. Haijalishi mazingira ya kimataifa yatabadilika namna gani, China siku zote itaiweka Afrika kama kipaumbele cha diplomasia yake, na siku zote inasimama kidete na mataifa ya Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



