Lugha Nyingine
Mwakilishi wa China katika UM apinga vikali shutuma potofu za baadhi ya nchi dhidi ya hali ya haki za binadamu nchini China
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei amepinga vikali shutuma za baadhi ya nchi dhidi ya hali ya haki za binadamu nchini China, na kujifanya walimu wa haki za binadamu bila kujali matatizo ya haki za binadamu katika nchi zao.
Balozi Sun amesema hayo katika hotuba yake ya kujibu shutuma potofu na zenye nia mbaya dhidi ya China zilizotolewa na baadhi ya nchi kwenye Mjadala Mkuu wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Balozi Sun amesema China inapinga vikali kauli ya wawakilishi wa Uingereza, Australia, Japan, Ireland, Czech, na Lithuania waliotoa shutuma zisizo na msingi na kukosoa hali ya haki za binadamu nchini China, akisisitiza kuwa China itaendelea kufuata njia ya maendeleo ya haki za binadamu inayoendana na mwelekeo wa nyakati na hali halisi ya nchi, na iko tayari kufanya mazungumzo ya kiujenzi na pande zote kuhusu masuala ya haki za binadamu, kupinga kwa pamoja mwelekeo wa kuyafanya masuala ya haki za binadamu kuwa ya kisiasa, na kufanya juhudi bila kusita ili kufikia lengo la kuhakikisha kila mtu ana haki za binadamu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



