Jukwaa la uvumbuzi Afrika latoa wito wa mtazamo unaojikita kwa vijana kuchochea mustakabali wa kidijitali

(CRI Online) Oktoba 01, 2026

Watunga sera, wataalamu na wafanyabiashara kutoka Afrika wametoa wito wa mtazamo unajikita kwa vijana ili kutengeneza mfumo ikolojia wa kidijitali ambao ni endelevu na jumuishi katika bara hilo.

Wito huo umetolewa wakati wa Tamasha la Uvumbuzi la Umoja wa Afrika la mwaka 2026 lililoanza jumanne wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Wanawake, Jinsia na Vijana katika Tume ya Umoja wa Afrika, Prudence Ngwenya amesema uvumbuzi hauhusiani tu na mawazo mazuri, bali pia unahusiana na watu, unahusiana kujenga mahusiano, na kutengeneza mfumo wa ikolojia na mawazo, na kuongeza kuwa, mawazo yanaweza kuwa suluhisho, suluhisho kuwa kiwanda, na kiwanda kutoa fursa kwa wengine.

Naye Kamishna wa Miundombinu na Nishati katika Tume hiyo Lerato Dorothy Mataboge ametoa wito wa juhudi za pamoja katika kukabiliana na vikwazo kadhaa vinavyozuia vijana kuendeleza kwa ufanisi mageuzi ya kidijitali barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha