Lugha Nyingine
Ghana yahitaji kuweka mikakati kutumia vizuri sera ya China ya ushuru sifuri
(CRI Online) Oktoba 01, 2026
Katibu mkuu wa Shirikisho la Waagizaji na Wauzaji wa Ghana Samson Asaki Awingobit, amepongeza sera ya ushuru sifuri ya China, akisema ni fursa muhimu sana kwa nchi za Afrika.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Awingobit amesema sera hiyo inawapatia wafanyabiashara wa Ghana kitu walichokuwa wakikitamani kwa muda mrefu, kwani inawapa fursa ya kuingia katika soko la China bila ya kulipa ushuru.
Amesema angependa kuona bidhaa zaidi za Ghana zikiingia katika soko la China, hivyo Ghana inapaswa kutafuta uelewa wa soko la China ili kujua bidhaa gani kutoka nchi hiyo zinahitajika sana katika soko la China.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



