Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania aahidi ushirikiano wa karibu zaidi na China

(CRI Online) Oktoba 01, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Mahmoud Thabit Kombo, amepongeza urafiki na ushirikiano uliodumu kati ya Tanzania na China, akithibitisha tema ahadi ya Tanzania ya kuinua uhusiano huo katika ngazi mpya.

Akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China Oktoba Mosi, Kombo amesema urafiki kati ya Tanzania na China umejengwa kwenye msingi imara, akizungumzia miradi mikubwa ya ushirikiano ikiwemo Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na mchango wa timu za madaktari wa China katika sekta ya afya nchini Tanzania.

Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema, China na Tanzania zimedumu kuwa marafiki wa kuaminiana na wenzi wa kutegemeka tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasua mwaka 1964, akielezea uhusiano huo kama mfano wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha