Lugha Nyingine
China yasema Japan haiwezi kuamua kujadili umiliki wa silaha za nyuklia
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Guo Jiakun amesema, suala la kumiliki silaha za nyuklia sio jambo ambalo Japan inaweza kuamua kulijadili au kutolijadili.
Guo amesema hayo kufuatia kauli zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Ulinzi wa Japan Shinjiro Koizumi kuhusu umiliki wa silaha za nyuklia, ambapo alisema majadiliano kuhusu umiliki wa silaha za nyuklia na nyambizi zinazotumia nishati ya nyuklia hayapaswi kuondolewa mezani wakati wa marekebisho ya "nyaraka tatu za usalama".
Guo amesema, Japan ni nchi isiyo na silaha za nyuklia na ni mshiriki wa Mkataba wa Kutoeneza Silaha za Nyuklia (NPT), na kwamba wajibu wa kutokubali, kutotengeneza, kutomiliki, au kutokueneza silaha za nyuklia ni wa kisheria na wa lazima chini ya sheria za kimataifa, na hauruhusu majadiliano yoyote ya kubadili msimamo huo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



