Lugha Nyingine
Hafla ya maadhimisho ya miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China yafanyika Beijing

(Picha/Xinhua)
Hafla ya maadhimisho ya miaka 77 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China imefanyika usiku wa tarehe 30 katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais wa China Xi Jinping.
Katika hotuba yake, rais Xi amesisitiza kuwa kupitia uchunguzi na utekelezaji wa muda mrefu, mfumo wa ujamaa wenye umaalumu wa China umeonyesha faida kubwa, mfumo wa utawala na uwezo wa utawala wa China umezidi kuimarika, na ustawi wa taifa la China umekuwa mwelekeo wa kihistoria usioweza kuzuilika.
Rais Xi pia ameeleza kuwa, katika miaka 77 iliyopita, Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeunganisha na kuongoza wananchi kufanya juhudi bila ya kusita, na kupata mafanikio mawili makubwa ya kutimiza maendeleo ya kasi ya uchumi, na kutimiza utulivu wa muda mrefu wa jamii. Pia kufikia lengo la kwanza la karne la kujenga jamii yenye maisha bora, na kupiga hatua ya kutimiza lengo la pili la karne la kujenga nchi kubwa ya kisasa ya kijamii katika pande zote.
Amesema China inajivunia mafanikio hayo yaliyopatikana na China mpya, na pia ina imani kubwa juu ya mustakabali mwema wa ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China.

(Picha/Xinhua)

(Picha/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



