IRGC yaonya kuwa Iran itatumia silaha mpya kama mgogoro utachukua sura nyingine

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2026

Msemaji wa Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Hossein Mohebbi, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, tarehe 29 Septemba 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Hossein Mohebbi, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, tarehe 29 Septemba 2026. (Xinhua/Shadati)

TEHRAN - Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) vimeonya kwamba kama mgogoro dhidi ya Iran utachukua sura mpya, nchi hiyo bila shaka italeta silaha mpya kwenye uwanja wa vita.

Akizungumza jana Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari wa moja kwa moja mjini Tehran, msemaji wa IRGC Hossein Mohebbi amesisitiza juhudi endelevu za nchi hiyo katika kupanua uwezo wake wa ulinzi.

"Tunasanifu silaha mpya bila kuchoka, kuboresha zilizopo, na kuendelea kuzalisha silaha kwa wingi ili kuweza kujilinda. Tunatumia teknolojia kutoka kote duniani kutengeneza silaha zenye uwezo wa kulinda nchi yetu na watu wetu," amesema, huku akiongeza, "Kama migogoro itachukua sura nyingine, bila shaka tutaleta silaha mpya kwenye uwanja wa vita."

Ameorodhesha baadhi ya hatua za kihasama za Marekani dhidi ya Iran ndani ya miezi iliyopita, ikiwemo kulazimisha vita vya siku 40 vilevile vizuizi vya majini na angani, kuongeza shinikizo la kiuchumi, kuchochea "ghasia za mitaani" mwezi Januari na kuyapa silaha makundi yanayoipinga Iran yaliyopo kwenye mipaka ya kaskazini-magharibi na kusini-mashariki mwa nchi hiyo, akibainisha kuwa mipango hiyo yote ilikuwa imehukumiwa kufeli.

Mohebbi ameongeza kuwa "adui" bila shaka ana mipango mingine, akisema Iran inafahamu mipango hiyo na imejitayarisha kwa ajili yake, "na itaendelea kupata ushindi katika siku za baadaye."

Msemaji wa Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Hossein Mohebbi, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, tarehe 29 Septemba 2026. (Xinhua/Shadati)

Msemaji wa Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Hossein Mohebbi, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Tehran, Iran, tarehe 29 Septemba 2026. (Xinhua/Shadati)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha