Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini atangaza hatua za kukabiliana na uhalifu wa ukatili dhidi ya wanawake
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza jana Jumanne kwamba atachukua hatua mbalimbali za kukabiliana na uhalifu wa ukatili dhidi ya wanawake, na ameahidi kuchukua hatua za muda mrefu na zisizokoma, ili kuwezesha kila mwanamke na msichana nchini Afrika Kusini kuishi kwa uhuru, heshima na usalama.
Kwenye hotuba yake kwa njia ya televisheni katika mji mkuu wa utawala, Pretoria, Rais Ramaphosa ametangaza hatua hizo zenye pointi nne ambazo ni:
Kwanza; amemuagiza Waziri wa Polisi na Waziri wa Sheria kufanya ufuatiliaji wa nchi nzima wa kesi ili kubaini kesi zilizopo za mauaji, ubakaji na mashambulizi dhidi ya wanawake ambazo hazijatatuliwa, na kubainisha idadi ya kesi husika ndani ya siku 30, na kuandaa mpango wa kusukuma mbele uchunguzi wa kesi hizo ndani ya siku 90.
Pili; ameiagiza idara ya polisi na idara husika kutatua msongamano wa kesi zinazochunguzwa kwa utaalamu wa kibailojia zinazohusiana na ukatili wa kijinsia na kuwasilisha suluhisho ndani ya siku 60.
Tatu; ameziagiza serikali za mitaa kukamilisha utambuzi wa maeneo yenye hatari kubwa kwa usalama wa wanawake ndani ya siku 60 na kutatua maeneo yenye hatari zaidi zilizojificha ndani ya siku 90.
Na nne; ameziagiza idara husika kutoa kanuni za matumizi ya bidhaa zinazohusiana na pombe, na kuongeza udhibiti wa kiwango cha juu zaidi wa ukatili wa kijinsia unaohusiana na ulevi.
Tangu mwezi Julai mwaka huu, miili 11 ya wanawake imegunduliwa huko Ekurhuleni, mashariki mwa Johannesburg, jiji kubwa zaidi nchini Afrika Kusini. Wahanga wengi walikuwa wamefanyiwa vitendo vikali vya unyanyasaji wa kijinsia kabla ya kuuawa. Hakuna maendeleo makubwa yaliyopatikana katika uchunguzi wa polisi kuhusiana na kesi hizo zilizotajwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



