Xi asisitiza kusukuma mbele Mpango wa China ya Amani ili kulinda mambo ya kisasa ya China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 29, 2026

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amehimiza juhudi za kusukuma mbele Mpango wa China ya Amani kwenye kiwango cha juu zaidi, ili kuhakikisha ujenzi wa mambo ya kisasa ya China unafanyika kwa hatua madhubuti siku hadi siku. 

Kwenye mkutano uliofanyika jana Jumatatu mjini Beijing, Xi amesema katika maagizo yake kuwa tokea Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwaka 2012, maendeleo makubwa yamepatikana katika kujenga China ya usalama, na kuifanya China kuwa moja ya nchi zenye usalama zaidi duniani.

Amesisitiza kufanya juhudi za kuhimiza hali ya jumla ya usalama wa nchi, na kushikilia na kuimarisha uongozi wa Chama kwa mambo yote katika eneo hilo.

Pia ametoa wito wa kufanya juhudi za kutafuta maendeleo na pia kulinda usalama, kuimarisha uhakikisho wa kisheria, kutumia njia za kisayansi na teknolojia, pamoja na kuzuia na kupunguza hatari za aina mbalimbali katika nyanja husika; ili kuifanya nchi kuwa na usalama zaidi, jamii kuwa na utaratibu zaidi, utawala wenye ufanisi zaidi, na wananchi wataridhika zaidi.

Chen Wenqing, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na mkuu wa Kamati ya Siasa na Sheria ya Kamati Kuu ya CPC, alihudhuria mkutano huo na kusoma maagizo ya Xi, pia alitoa hotuba.

Chen amesema kuwa matokeo yameonesha kuwa, Pendekezo la China ya Amani limepata kutambuliwa duniani, na usalama umekuwa alama wazi ya utawala wa China.

Chen ametoa wito wa kutumia mbinu za kutoa adhabu na kufanya uzuiaji pia ili kuleta ufanisi wa pamoja, na amehimiza kufanya juhudi kubwa za kusukuma mbele Pendekezo la China ya Amani kwenye kiwango cha juu zaidi. 

Kwenye mkutano huo wa Jumatatu, miji 60 na wilaya 160 zimebainishwa kuwa vielelezo vya kusukuma mbele Pendekezo la China ya Amani na zimekabidhiwa tuzo za heshima.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha