Lugha Nyingine
Angalau watu 12 wafariki kwenye ajali ya mashua mashariki mwa DRC
(CRI Online) Septemba 28, 2026
Angalau watu 12 wamefariki na wengine wengi hawajulikani walipo baada ya mashua iliyokuwa imebeba abiria 80 kupinduka kwenye Ziwa Kivu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti jana Jumapili kwamba ajali hiyo ilitokea kati ya usiku wa Jumamosi na alfajiri ya Jumapili, na kwamba mashua hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Bukavu, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kusini, na kupinduka wakati wa safari hiyo.
Vyombo hivyo vikirejelea taarifa za awali vimeripoti kuwa waokoaji wamepata miili ya watu 12 na manusura watano hadi kufikia jana alfajiri, huku wengine wengi wakiwa bado haifahamiki hali yao. Aidha, shughuli za utafutaji na uokoaji zilikuwa bado zinaendelea.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



