Lugha Nyingine
Ofisa wa UN ahimiza ufadhili zaidi wakati tishio la El Nino likiongezeka katika Pembe ya Afrika
Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Dharura na Uhimilivu katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Rein Paulsen, ametoa wito wa kukusanya rasilimali ili kukabiliana na msukosuko unaozidi kuongezeka katika Pembe ya Afrika wakati tishio la hali ya El Nino likikaribia.
Akizungumza jijini Nairobi, Kenya, hivi karibuni, Paulsen amesema, ingawa serikali za kikanda zimeandaa mipango ya kukabiliana na hali hiyo, uhaba mkubwa wa fedha unatishia utekelezaji wa mipango hiyo.
Amesema ili kukabiliana na hali hiyo, Juni 18, FAO na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani zilizindua mpango wa pamoja wa kukabiliana na El Nino, unaohusisha nchi 22 barani Afrika, Asia na Pasifiki, Latini Amerika na Karibeani, unaohitaji dola za kimarekani milioni 202 kulinda watu milioni 8.8 walio katika mazingira dhaifu kwenye nchi hizo zilizo hatarini kutokana na hali mbaya zaidi ya hewa inayosababishwa na El Nino.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



