Iran yasema imejitayarisha kwa mapambano mapya na Marekani lakini haijaachana na diplomasia

(CRI Online) Septemba 28, 2026

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Bw. Abbas Araghchi amesema, Iran imejiandaa kwa kuanza upya kwa mapigano na Marekani lakini bado haijaachana na mazungumzo ya kidiplomasia.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Utangazaji la Marekani (NBC), Araghchi alisema, "Tuko tayari kabisa kwa kuanza upya kwa uhasama," huku akiongeza, "Pia tuko tayari kwa mazungumzo ya kidiplomasia wakati wowote." Alibainisha, "Inategemea uamuzi utakaofanywa na Rais wa Marekani Trump."

Awali, kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York tarehe 25, Araghchi alisema Iran imekabidhi mpango wa kufungua tena Mlango Bahari wa Hormuz kupitia Qatar, lakini Rais wa Marekani Donald Trump ameukataa mpango huo na kusema huenda atarejea kuishambulia Iran kwa mabomu baada ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa Bunge la Marekani utakaofanyika mwezi Novemba.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha