Lugha Nyingine
WHO yaonya kuwa homa ya Ebola nchini DRC bado haijadhibitiwa
Mkurugenzi wa mpango wa dharura wa Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Afrika Marie Roseline Belizaire Jumatano amesema licha ya kuwepo kwa dalili za unafuu katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika, mlipuko wa homa ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) bado haujadhibitiwa, ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa katika mkoa wa mashariki wa Kivu Kaskazini.
Kwa mujibu wa idara za afya nchini DRC, hadi Septemba 21 wagonjwa 7,773 wamethibitishwa nchini humo, na 3,759 kati yao wamefariki.
Belizaire amesema dalili za kwanza za kutia moyo zimeanza kuonekana. Kuanzia tarehe 31 Agosti hadi tarehe 20 Septemba, idadi ya wagonjwa mkoani Ituri imepungua kwa takriban asilimia 26, na mkoani Haut-Uele imepungua kwa takriban asilimia 15. Hata hivyo, idadi ya wagonjwa huko Kivu Kaskazini imeongezeka kwa asilimia 73 kwenye kipindi hicho, ikiashiria kwamba janga hilo bado halijadhibitiwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



