Lugha Nyingine
Vikosi vya wapiganaji wa Tigray nchini Ethiopia wafanya mashambulizi na kutwaa viwanja vya ndege
Kwa mujibu wa mshauri wa Waziri Mkuu wa Ethiopia anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki, Getachew Reda, vikosi vya wapiganaji wa Tigray (TPLF) vimeanzisha mashambulizi makali dhidi ya ngome za serikali ya Ethiopia katika maeneo ya Afar na Amhara, na kutwaa viwanja vya ndege vilivyokuwa chini ya udhibiti wa serikali kuu huko Tigray.
Shirika la Ndege la Ethiopia limesimamisha kwa muda safari za ndege za kwenda Mekelle, Axum na Shire katika eneo la Tigray nchini humo, kuanzia siku ya Jumatano, kutokana na hali ya sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, kusimamishwa kwa safari za ndege kunakuja wakati ambao mivutano huko Tigray inaongezeka, kufuatia tangazo la Jumapili kuhusu muungano mpya wa makundi saba ya upinzani na makundi yenye silaha nchini Ethiopia.
Pande hizo hasimu zilisaini makubaliano ya amani Novemba 2022, hatua iliyomaliza uhasama na kuwezesha Shirika la Ndege la Ethiopia kurejesha safari zake kwenda maeneo ya Tigray baada ya kusitisha kwa zaidi ya mwaka mmoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



