Rais wa Sudan Kusini avunja serikali ya mpito kabla ya uchaguzi wa mwezi Desemba

(CRI Online) Septemba 24, 2026

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, amevunja serikali ya mpito Jumanne jioni, kabla ya uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwezi Desemba.

Amri hiyo ya rais ilivunja bunge la taifa na serikali za majimbo ya Sudan Kusini, ikiwaondoa madarakani makamu wa kwanza wa rais na makamu wengine wanne wa rais, pamoja na kuteua serikali ya muda wa kusimamia kipindi cha kuelekea uchaguzi wa tarehe 22 Desemba, ambao umeshaahirishwa mara mbili.

Riek Machar, ambaye anashikilia wadhifa wa makamu wa rais wa kwanza, amesimamishwa kazi tangu Septemba 2025 na anakabiliwa na kesi kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uhaini.

Amri hiyo ya rais, iliyotangazwa kupitia shirika la utangazaji la kiserikali la Sudan Kusini, ilieleza kuwa Kiir ataendelea kuwa rais katika kipindi chote cha uchaguzi hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa na kuapishwa. Nazo mahakama na taasisi za usalama zitaendelea na majukumu, huku washauri na wajumbe wa rais wataendelea kuhudumu moja kwa moja chini ya mamlaka ya Kiir.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha